Mwanaume Amshitaki Mke kwa Kujifungua Mtoto Mwenye Sura Mbaya, Hakimu Aagiza Mke Amlipe Mume $120,000 [PICHA]


Jamaa mmoja aliyefahamika kwa jina la Jian Feng, hivi karibuni alimshitaki mke wake kwa kujifungua kile alichokiita “mtoto mbaya wa kike.”

“Nilimuoa mke wangu pasipo na mapenzi, ila muda mchache baada tulipata mtoto wetu wa kike na maisha yakaendelea,” jamaa aliieleza Irish Times.


“Mtoto wetu alikuwa ni mbaya sana, kufikia kiasi alikuwa ananitisha hata mimi.”

Jian anamtuhumu mke wake sababu anafahamu kwamba yeye asingeweza kuwa baba mzazi wa mtoto huyo asiyevutia.
 

Chakushangaza ni kwamba, vipimo vya DNA vilithibitisha kuwa mtoto kweli ni wake, ila baadae mke wake akaja na kusema ukweli kwamba siku za nyuma aliwahi kutumia kiasi cha $100,000 zilizoweza kumsaidia kufanya upasuaji wa sura yake ambao ulifanyika nchini Korea ya Kusini kabla hawajakutana.

Feng amemshitaki mke wake kwa uongo alioufanya, kwa kutomwambia ukweli juu ya kufanyiwa upasuaji wa marekebisho ya sura yake, kitendo kilichompelekea kuamini kwamba mke huyo alikuwa mzuri.


Hakimu alikubali hoja ya Feng na kumtaka mke wake amlipe kiasi cha $120,000 kama fidia.

No comments:

Post a Comment