Chelsea Bado Wanamlipa Di Matteo £130,000 kwa Wiki Licha ya Kuwa Walishampiga Chini Mwaka Mmoja Uliopita


Roberto Di Matteo bado anaendelea kulamba £130,000 kwa wiki toka timu ya Chelsea licha ya kuwa alishapigwa chini miezi 12 iliyopita.

Muitalina huyo alishindwa kufikia makubaliano na mmiliki wa timu hiyo Roman Abramovich juu ya mkataba wake wa miaka mitatu ambao walikubaliana hapo awali, hii ikiwa ni miezi sita tu mara baada ya kutwaa taji la Champions League kama kocha wa muda.

Mpaka sasa Di Matteo ameshaweka kibindoni kiasi £7million na bado ataendelea kupokea mshahara mpaka mwezi June 2014, anatakiwa asiingie kwenye mkataba na timu nyingine kinyume na hapo mkataba na Chelsea unakuwa umevunjika rasmi.


No comments:

Post a Comment