Bolt na Fraser-Pryce Washinda Tuzo za Mwaka kwa Ukimbiaji


Mnamo siku ya Ijumaa wakimbiaji toka nchini Jamaica Usain Bolt na Shelly-Ann Fraser-Pryce walitangazwa kuwa wakimbiaji bora wa mwaka huu na Shirikisho la Kimataifa la Mchezo wa Mbio (IAAF).

Bolt alishinda tuzo hiyo kwa mara ya tano na hii ni baada ya kulitetea vyema taji lake la mbio za mita100, huku akishinda mbio za mita 200 kwenye fainali za 2013 zilizofanyika jijini Moscow na kuweka rekodi mpya ya kukimbia kwa sekunde 19.66 kwenye mashindano ya Dunia yaliyoandaliwa na IAAF.

Mjamaica mwenzake, Fraser-Pryce, alishinda tuzo hiyo kwa upande wa wanawake iki ni mara yake ya kwanza, hii ni mara baada ya kufanikiwa mbio za mita 100 kwenye mashindano hayo ya Dunia akifanikiwa kumaliza ndani ya sekunde 10.17 muda ambao unabaki kuwa wa juu ndani ya mwaka huu. Pia alishinda mbio za mita 200 zilizofanyika jijini Moscow.



No comments:

Post a Comment