Afrika Kusini Yawafunga Mabingwa wa Dunia Hispania


Mabingwa wa Kombe la Dunia timu ya taifa ya Hispania wamejikuta wakipokea kipigo cha pili kati ya mechi 17 walizocheza mara baada ya kufungwa na Afrika ya Kusini kwenye mechi ya Kimataifa ya kirafiki iliyochezwa hapo jana.

Kiungo wa timu ya Afrika Kusini Bernard Parker alifanikiwa kufunga goli la ushindi ikiwa ni mapema ndani ya kipindi cha pili, akiu-chop mpira uliompita kipa wa Hispania Victor Valdes.

No comments:

Post a Comment