Rihanna Ayasikilizia Maumivu Makali kwa Ajili ya Tattoo (PICHA)

Rihanna Akiwa Anachorwa Huku Akisikilizia Maumivu
Hapo jana mchoraji nguli wa michoro ya tattoo toka nchini New Zealand aitwaye Inia Taylor aliziweka picha zinazomuonyesha Rihanna akiwa anachorwa tattoo za kudumu za kiasili zinazojulikana kama Maori tattoo kwenye mkono wake wa kulia.

Maori tattoo ni moja kati ya tattoo ambazo huwa zinauma sana pindi zinapokuwa zinachorwa kwenye ngozi, sababu zenyewe huwa hazitumii sindano zilizozoeleka, aina hii ya tattoo huwa zinatumia wino maalumu na nakshi nyingine.....Tofauti na tattooo za kisasa zilizozoeleka kukaa juu ya ngozi zenyewe huwacha ngozi ikiwa na alama ya kudumu.

Alichora tattoo hizo akiwa New Zealand baada ya kumaliza ziara yake ya kimuziki anyoizunguka Dunia.

Mcheki Rihanna akiugulia maumivu.....

Anaonekana Yupo Strong

Mchoro Kamili

No comments:

Post a Comment