Mimi Msichana mwenye Umri wa miaka 23..
Nimekuwa kwenye mahusiano na mume wa dada yangu kwa mda wa miaka mitano sasa bila dada yangu kufahamu.
Kuna wakati huwa tunakaa pamoja yaani mimi, dada yangu na mme wake, ila wakati mwengine huwa naamua kukaa mbali nao kutokana na hali ya kujishtukia.
Mahusiano yetu yalianza kipindi nilipomaliza elimu ya sekondari uhusiano unaoendelea mpaka sasa nikiwa chuo.
Sijui hata ilitokeaje ila nimejikuta nikiingia kwenye mapenzi mazito sababu yeye ndiye aliyekuwa mwanaume wangu wa kwanza, na mpaka sasa nampenda naye ananipenda sana, na hivi sasa nipo kwenye hatua za mwisho za kumaliza chuo huku miezi michache ikiwa imebaki.
Nimemwambia inabidi tuvunje mahusiano sababu sitaki dada yangu afahamu juu ya hili ila yeye anasisitiza kuwa anataka kunioa mimi. Nimechanganyikiwa kwa sasa sababu nahitaji nitulie baada ya masomo yangu.
Je nifanyeje kuwafanya watengane..?
No comments:
Post a Comment