Matonya a.k.a Tonya |
Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa kiazi kipya nchini Matonya a.k.a Tonya Time, hivi karibuni alijikuta anashindwa kuhimili machungu yake kiasi cha kujikuta akitumia lugha isiyo rasmi wakati akiwa anafanya mahojiano live kwenye kipindi cha The Takeover kinachorushwa na kituo cha TBC fm.
Hali hiyo ilitokea mara baada ya mimi kumuliza kama kuna watu wanahusika kukwamisha maendeleo ya muziki wake, na wakati anajibu swali hilo huku akionekana kuwa na uchungu juu ya jambo hilo, Matonya alijikuta akisema neno la kizungu F**k kutokana na kuona kukwazwa na watu alioshindwa kuwataja.
"Kuna watu wapo kwa ajili ya kuziba riziki za wenzao ila mimi nasimama kupambana nao ila inasikitisha sana kwa nini iwe hivi... f**k" alisema Matonya.
Kwa sasa Matonya ana wimbo mpya ambao siku hiyo alifika studio kuuzindua rasmi, wimbo unaokwenda kwa jina la UTATA.
Kwa sasa Matonya ana wimbo mpya ambao siku hiyo alifika studio kuuzindua rasmi, wimbo unaokwenda kwa jina la UTATA.
No comments:
Post a Comment