Julius Nyaisangah "UNCLE J" Afariki Dunia

Julius Nyaisangah "Uncle J"
Habari zilizonifikia toka mkoani Morogoro na kuthibitishwa na watu wa karibu zinasema kwamba Mtangazaji Mkongwe nchini wa TV na Radio, Julius Nyaisangah maarufu kama 'Uncle J' amefariki dunia leo asubuhi.

Meneja wa kampuni ya Abood Media aitwaye Abeid Dogoli amethibitisha juu ya kifo hicho, huku akisema kwamba Marehemu alipelekwa hospitali ya Mazimbu jana majira ya saa nane mchana kutokana na kusumbuliwa na Kisukari pamoja na presha na asubuhi ya leo akafariki.
 
Marehemu amefariki akiwa na umri wa miaka 53 na alikuwa ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Abood Media, aliwahi kufanya kazi katika kituo cha Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na kampuni ya IPP Media Group ambapo alikuwa Mkurugenzi wa kituo cha Radio One.

Taarifa za awali zinasema mara yake ya mwisho Marehemu kuingia kuingia ofisini ilikua juzi japokuwa alikuwa yupo likizo kuanzia tarehe 12 Oktoba.

Mungu Ailaze Roho ya Maremu Nyaisangah Mahali Pema Peponi....

No comments:

Post a Comment