Dola Indidis |
Serikali ya nchi ya Israel imefikishwa mahakamani na Wakili mmoja wa Kenya kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, International Criminal Court of Justice (ICJ), kwa kosa la kumtesa na kumuuwa Yesu Kristo, kitendo ambacho Wakili huyo anadai kilikuwa ni kinyume na sheria, kwa mujibu wa taarifa ya vyombo vya habari.
Wakili huyo wa Kenya aitwaye Dola Indidis anadai Waisrael na Wayahudi wanahusika moja kwa moja na kuhusika na kifo cha Yesu Kristo na inatakiwa washtakiwe kisheria, hii ni kwa mujibu wa Jerusalem Post.
Indidis, ambaye ameipeleka kesi hiyo ICJ ndaini ya The Hague, pia anawashitaki Tiberius, kiongozi wa Rome wa mwaka 42 BCE, “Pontius Pilate, baadhi ya viongozi wa Kiyahudi, Mfalme Herod, Serikali ya Italia, na Serikali ya Israel,” kwa mujibu wa Gazeti hilo.
Indidis anatumia Biblia kama ushahidi wake wa kwanza kwenye kesi hiyo.
“Ushahidi kwa sasa upo kwenye kumbukumbu za Biblia, na huwezi kuipinga Biblia,” Indidis alinukuliwa akisema kupitia taarifa ya habari ya Citizen.
Indidis pia akasisitiza “Serikali ya Israel ambayo ipo madarakani ndiye mshtakiwa wa kwanza kwenye kesi hiyo,” taarifa hiyo ilisema.
No comments:
Post a Comment