Mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama Kutoa Album ya Hip Hop

Michelle Obama
Michelle Obama anategemea kuachia album ya hip hop. Na hapa ni hivi, hapana, ila yeye hautomsikia akishuka mistari.
 
Katika jitihada zake mfululizo wa kupigania matizo ya watoto kupitia kampeni inayoitwa “Let’s Move!”, First Lady huyo ameungana na vikundi vya Healthier America na Hip Hop Public Health Foundation ili kuzindua album hiyo yenye mchanganyiko wa wasanii watakaotoka na album yenye nyimbo 19, huku lengolikiwa ni kuwashawishi watoto kujifunza namna nzuri kuchagua vyakula vyenye afya.

Wasanii kama Run DMC, Ashanti, Doug E. Fresh, Monifah na mshindi wa shindano la American Idol Jordin Sparks wote wanashiriki kuchangia sauti zao kwenye album hiyo ambayo itaitwa Songs for a Healthier America.

No comments:

Post a Comment