Genevieve ni Mwanamke Mkali Ndani ya Nollywood Asema Ramsey Noah

Genevieve na Ramsey Noah
Ni wangapi waliwahi kusikia au kuhisi kwamba waigizaji maarufu wa filamu toka Nigeria Ramsey Noah na Genevieve Nnaji kwamba walishawahi kuwa kwenye mahusiani, je uliamini au hukuamini?

Hivi karibuni alipokuwa anafanya mahojiano, Ramsey alifunguka kwa kauli iliyozidi kuwachanganya watu juu ya ukweli kuhusiana na jambo hilo, ya kwamba hakunaga mwanamke mkali na bomba miongoni mwa waigizaji wanawake wa Nigeria kama yeye, "Genevieve ni mwanamke mkali ndani ya Nollywood" alisema Ramsey.

Kwani uzuri wa mtu ni upi hasa, sura na umbo lake au mambo ya ndani?

Kwenye mahojiano hayo pia alizungumzia kuhusiana na ndoa yake na kipindi ambacho alikwama nyumbani kwake kwa siku tatu baada ya kukutana na mwanamke aliyemwambia kuwa ametumwa na Mungu aje kuolewa naye.

No comments:

Post a Comment