Watoto 22 Wafariki Baada ya Kula Chakula Chenye Sumu


Jumla ya watoto 22 wameripotiwa kufariki na wengineo wengi wakiwa wanaumwa mara baada ya kula chakula cha mchana shuleni kwao kinachosadikiwa kuwa kilikuwa na sumu ya kuuliwa wadudu, maafisa wa India wamesema leo.

Haijawekwa wazi ni kwa namna gani madawa hayo ya sumu yaliingia kwenye chakula cha mchana kinachotolewa na shule hiyo iliyopo Mashariki mwa jimbo la Bihar, japo maafisa hao wamesema kwamba kuna uwezekano chakula hicho kilikuwa hakijasafishwa vizuri kabla ya kupikwa.


Watoto kati ya umri wa miaka 8 na 11,  walijisikia wanaumwa mara baada ya kula chakula chao cha mchana ndani ya Masrakh, kijiji kilichopo maili 50 kaskazini mwa jimbo la makao makuu ya Patna. 



No comments:

Post a Comment