Chelsea Yatoa £10m na Mchezaji Mmoja Kati ya Mata au Luiz Ila Manchester Yakataa Kumuuza Rooney

Manchester United wamekataa ofa ya kwanza ya Chelsea kwa mchezaji wao Wayne Rooney, ofa ya kiasi cha paundi millioni 10 sambamba na mchezaji mmoja.

Gazeti la Sportsmail linaamini miongoni mwa wachezaji wawili mmoja wao alihusishwa kwenye dili hilo, mmoja akiwa mchezaji wa mwaka wa Chelsea Juan Mata au mlinzi wa kati toka Brazil David Luiz.

United wamesisitiza kwamba Rooney hauzwi na bosi wa Chelsea Jose Mourinho anatakiwa kuamua upya kutangaza ofa kwa mchezaji huyo.

No comments:

Post a Comment