Mkongwe Kwenye Muziki KIbibi Tina Turner Kuolewa Akiwa na Miaka 73

Tina Turner na Erwin Bach
Nani anayesema mapenzi ya kweli huwa yanakingamana na umri?
 
Mwanamuziki mashuhuri na mkongwe, Tina Turner anategemea kupanda tena altaleni akiwa na umri wa miaka 73 sasa.
 
Kwa mujibu wa taarifa, mwanamuziki huyo na mpenzi wake, Erwin Bach wanajiandaa kufunga pingu za maisha ndani ya Lake Zurich nchini Switzerland mnamo 21, July (Siku ambayo pia ni kuzaliwa kwa Dan Chibo).

Mahusiano ya Tina na Bach, 57, yalianza wenye kipindi ambacho jamaa alikuwa ni kiongozi kwenye lebo ya utayarishaji yamwanabibi huyo, na wapo kwenye mahusiano toka mwaka 1986 na wamekuwa wakiishi ndani ya Switzerland toka mwaka 1994.

No comments:

Post a Comment