Nyota wa muvi ya Flight, Denzel Washington ambaye amekuwa kwenye ndoa kwa muda wa miaka 30, hivi karibuni ameingizwa kwenye kashfa nzito kutokana na picha inayomuonyesha akiwa anambusu mwanamke mwengine, mtandao wa RadarOnline.com umeanika hayo.
Denzel, 58, na mke wake Pauletta, 62, hivi karibuni walifanya mahojiano na jarida la Ebony ambapo walizungumzia juu ya ndoa yao ya muda mrefu huku picha yao ikiuza jarida hilo kwa kukaa ukurasa wa mbele.
Ila kwa sasa picha nyingi zimekuwa zikitapakaa kwenye mitandao ambazo zinamuonyesha Denzel akiwa anambusu mwanamke mwengine kwenye lips zake, katika kile kilichotafsiriwa ni usaliti juu ya mke wake.
No comments:
Post a Comment