Kutana na Mgahawa Ambao Wahudumu Wake Wanahudumia Bila Kuwa na Nguo


Mgahawa mmoja imebidi ujipange na kuamua upi utakuwa uamuzi wake mara baada ya jiji kuusimamisha kutokana na kitendo chake cha kuruhusu wahudumu wa kike kutumia michoro mwilini mwao badala ya nguo kama ndiyo sare yao wakati wanahudimia wateja.

Baada ya malalamiko kufika polisi juu ya kitendo hicho cha wahudumu wa wa mgahawa huo wa Redneck Heaven, ulipo ndani ya jimbo la Texas, mamlaka ya jiji waliamua kubadili sheria zake, huku zikikataza wanawake kuficha matiti yao kwa kutumia michoro.

Mwanamke mmoja kwenye kikao kimoja cha halmashauri hiyo ya jiji, kilichofanyiaka siku ya Jumatatu alitoa hoja juu ya kitendo hicho.

“Tunashtushwa sana kuona hawa waschana wadogo hawavai nguo,” Catherine Holliday alisema.


CHANZO: Huffington

No comments:

Post a Comment