INATISHA: Mafuvu 56 ya Vichwa vya Watu Yakutwa Nyumbani kwa Mtu


Police wa Austria kwenye jimbo la Burgenland inamshikilia jamaa ambaye amekutwa na mafuvu 56 ya vichwa vya watu pamoja na baadhi ya mifupa ya viungo vya binadamu nyumbani kwake.

Shirika la Umma la Utangazaji nchini humo ORF limetoa taarifa hiyo mnamo siku ya Jumanne, likisema kuwa mafuvu hayo yalichukuliwa na jamaa huyo toka kwenye makaburi ya Kanisa moja.

Pia limetaarifu kwamba, polisi walipatwa na wasi mara baada ya kumuona jamaa huyo mwenye umri wa miaka 47 akiuza mafuvu matatu na mifupa miwili ya miguu kwenye soko moja.

CHANZO: Huffington Post

No comments:

Post a Comment