Kiduku, Kwaito na Azonto Ndani ya Kanisa ni Sahihi Ama...?
Je kuna aina maalumu ya muziki au mitindo ambayo inatakiwa kutumika kucheza na kuimba kwa ajili ya kusifu na kuabudu pekee?
Basi kama ni hivyo na tuwaambie watu wa Afrika Kusini waache kuwa wanaimba Kwaito au mitindo yao mengine Makanisani, waambieni na watu wa Amerika ya Kusini waache kuimba nyimbo za Samba kama nyimbo zao za kusifu.
Ninachokiona mimi hapa ni Roho zaidi ndiyo inayohusika.
Kwa maana unaweza ukawa hauimbi Hip Hop au Bongo Fleva, ila ukweli ni kwamba Moyo wako sio safi, ila kuna mtu anaimba Bongo Fleva , Hip Hop au hata Regge kwa moyo wake wote, huku fikra na mawazo yake yakiwa wazi juu ya Mungu wake....
Kwa hili, binafsi nina hakika baraka za Mungu na matunda yake yatumuangukia...
Ipi ni Imani yako juu ya hili...?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment