Halle Berry Kuolewa kwa Mara ya Tatu

Halle Berry
Mcheza filamu maarufu toka nchini Marekani mwanadada Halle Berry, ametangaza kuwa ataolewa na mchumba wake, Oliver Martinez, mwishoni mwa juma hili.

Berry, ambaye awali aliwahi kusema kwamba hatokuja kuolewa tena, amesema alijikuta amepatwa na mshangao baada ya kuchumbiwa na mcheza sinema huyo toka Ufaransa.

Baada ya kuchumbiwa na Olivier ambaye walikutana mwaka 2012,Berry alikuja kutania kwa kusema  akisema, "nani alijua?! naipotezea, sio? Usiseme haiwezekani, watu wangu!"

Wawili hao wamechumbiana toka mwezi March, 2012 na kuifanya hii kuwa ni ndoa ya tatu kwa Berry, ambaye mwanzoni aliwahi kuolewa na David Justice mwaka 1991 na mwanamuziki Eric Benet mnamo mwaka 2001.

No comments:

Post a Comment