Familia ya Kifalme Yategemea Kupata Mtoto, Catherine Yupo Chumba cha Uzazi


Catherine, Duchess wa Cambridge
Catherine, Duchess wa Cambridge yupo kwenye hatua za awali mara baada ya kufikishwa hospitali majira ya saa 12 asubuhi akiwa kwenye mandalizi ya kujifungua kwa yule atakajekuwa Mfalme au Malkia wa baadae.

Duke wa Cambridge, Prince William akiwa na mke wake walisafiri kwa gari kutoka Kensington Palace mpaka Lindo Wing kwenye hospitali ya St. Mary iliyopo ndani ya Paddington, Magharibi ya jiji la London, sehemu ambayo yeye alizaliwa mnamo mwaka 1982.

"Duchess wa Cambridge amepelekwa hospitalini hapo asubuhi ya leo kwenye hospitali ya St. Mary Hospital, Paddington, London kwenye hatua za mwanzo za kujifungua," msemaji wa familia hiyo ya kifalme alisema.
Waandishi wa Habari nao walikuwepo Hospitali hapo

No comments:

Post a Comment