Cristiano Ronaldo Atastaafu Akiwa Real Madrid, Asema Rais wa Klabu

Cristiano Ronaldo
Cristiano Ronaldo atamalizia mpira wake akiwa Real Madrid, hii ni kwa mujibu wa Rais wa klabu hiyo Florentino Perez.

Mreno huyo mwenye umri wa miaka 28, hivi karibuni amekuwa akihusishwa na tetesi za kurudi Manchester United au kwenye uhamisho wa watumia hela wa Ufaransa klabu ya Monaco.
 
Ila Perez alisema: "Unatakiwa uwe na uhakika kwamba Cristiano atastaafu akiwa Real Madrid."

Akaongeza pia kwamba Real hawajatoa ofa yoyote kwa mchezaji wa Spurs' Gareth Bale, wala hawajapokea ofa toka Arsenal kwa ajili ya Gonzalo Higuain.

No comments:

Post a Comment