Brazil Watwaa Confederations Cup - Waipiga Hispania 3-0

Neymer Akiwa na Kombe
Brazil wamefanikiwa kutwaa kombe la Confederations baada ya kuwafunga Mabingwa wa Dunia na Ulaya timu ya Hispania kwa magoli 3-0 kwenye fainali iliyoonekana kuwa ni ya upande mmoja iliyofanyika kwenye uwanja wa Maracana.

Fred alifunga mara mbili na Neymar mara moja huku Brazil wakionekana kuutawala mchezo kwenye usiku ambao ulikuwa ni mbaya kwa Wahispania hao, huku wakikosa penati na wakimaliza mchezo wakiwa wachezaji kumi uwanjani.

No comments:

Post a Comment