Mwanamke Apigwa Mpaka Kufa kwa Kumruhusu Mtoto wa Kike Kuvaa Jinzi


Kwenye mazingira ya kushanganza nchini India, mama mmoja ameuwawa baada ya kumruhusu mwanae kuvaa suruali ya jeans.

Mwamke huyo mwenye umri wa miaka 55 aitwaye Kamlesh Dubey alitolewa toka ndani ya nyumbani kwake na kuanza kupigwa na kundi la watu mara baada ya kutokea kwa majibizano ambaye alikuwa anapinga kitendo cha msichana huyo aitwaye Gunjan kuvaa jinzi kitu ambacho ni kinyume na mila za ki-sari.

Majibizano hayo yaliendelea na hata Gunjan, 20, na baba yake Netrapal walijeruhiwa kwenye ugomvi huo ambao ulitokea kwenye jiji la Aligarh ndani ya Uttar Pradesh, taarifa ya IBI Times imeeleza.

No comments:

Post a Comment