Shetta Hoi Akiwa Amelazwa


Shetta Akiwa Amelazwa
Msanii mkali wa muziki wa kizazi kipya Nurdin Bilali maarufu kama Shetta ni mgonjwa akiwa amelazwa kwenye Hospitalia ya Dr. Ameer jijini Dar, kwa sasa msanii huyo amelazwa akiwa hoi akisumbuliwa na ungonjwa wa Maralia.
Shetta anayetamba na ngoma ya Sina Imani alinieleza, hali yake ilikuwa mbaya sana ila kwa sasa ana nafuu japo bado bado amelazwa katika hospitali hiyo iliyopo maeneo ya Kariakoo jijini huku akiwa maetudikwa dripu.
alipoongea na mimi kwa njia ya simu Shetta alisema, tangu wiki iliyopita alikuwa anajisikia vibaya, hali yake ilibadilika gafla na kuwa mbaya zaidi siku moja mara baada ya kutoka kufanya show kwenye moja kati ya kumbi za jijini Dar.
“Hali ilikuwa sio nzuri, ila namshukuru Mungu kwa maana sijawahi kujisikia vibaya kama ambavyo nimejisikia pindi nilipoletwa hapa, ila kwa sasa najisikia nafuu zaidi mara baada ya kupata matibabu, nililetwa hapa siku ya Jumamosi na sikuwa kwenye hali nzuri hata kidogo” alisema Shetta.
Wakati anafanyiwa vipimo Shetta alionekana kuwa na Maralia tano,  ndipo ilipobidi aanzae dozi huku akitundikiwa dripu mfululizo za maji.
Akiongea kwa sauti ya chini Shetta alinieleza “hivi niniavyoongea na wewe ndio nimepata hata nguvu ya kupokea simu, maana nilikuwa nipo nje ya mawasiliano kwa siku mbili sasa, na hii ni kutokana na hali mbaya niliyokuwa nayo, namshukuru Mungu kwa maana naendelea vizuri, na hali ikiendelea kuwa hivi naweza kuruhusiwa kutoka” alisema Sheta.
Ugua Pole Shetta…..,

No comments:

Post a Comment