Mchezaji Shoga Wa NBA Jason Collins, Aanza Kupokea Vitisho Vya Kuuliwa Baada Ya Kujitangaza

Jason Collins
Jamaa wa kwanza ambaye amejitokeza na kuweka wazi kwamba yeye ni shoga, kwenye michezo ya ligi kuu nchini Marekani, Jason Collins, ambaye alisanuka na kuongea mnamo siku ya Jumatatu, ameanza kupokea vitisho vya kuuliwa na baadhi ya watu kupitia kwenye twitter na mitandao mengine ya kijamii.

Mnamo siku ya Jumatatu, Collins alizungumza kuhusu hali yake na kukiri kwamba yeye ni shoga kupitia jarida moja la michezo.


Alisema: “Mimi ni mchezaji wa kati wa NBA nikiwa na umrri wa miaka 34, ni mweusi na ni shoga.”

Kwenye twitter watumiaji waliandika: ”Jason collins toka nje ya kabati! Uwa malaya mbwa!!! @nba lol”.


Mwengine akasema: “Kitendo cha kusikiliza Jason Collins akijielezea kwamba yeye ni shoga kama vile ni kitu kizuri, kinanifanya kutaka kutapika. Na kumuuwa.”

No comments:

Post a Comment