Hulk Hogan Afungua Kesi Ya Madai Kutokana Na Kuvuja Kwa Mkanda Wake Wa Ngono

Hulk Hogan
Hulk Hogan ameamua kufungua kesi ya madai dhidi ya mtandao mmoja na rafiki yake, madai ya kiasi cha dola milioni 100 baada ya mkanda wake wa ngono kuingizwa kwenye mtandao, hii ni kwa mujibu wa taarifa.

Taarifa hiyo imeongeza kwa kusema Hulk Hogan aliwahi kufanya ngono na mke wa rafiki yake kipenzi miaka sita iliyopita na bila ya yeye kujua jamaa alikuwa anamrekodi kwa siri.
 
Toka video hiyo ivuje kwenye mtandao, Hogan amekuwa wa kijana na mwenye hasira hivyo kuamua kumfungulia rafiki yake na mtandao uliohusika kesi ya madai ya dola milioni 100.
 
"Bwana Hogan ana haki na uhuru wa mambo yake ya ndani, kama walivyo Wamarekani wengine walio na haki ya uhuru wa mambo yao ya vyumbani mwao," Wakili wa Hogan aitwaye Charles Harder alisema.

Jamaa yake, Bubba the Love Sponge Clem, alikana kuhusika na kuivujisha video hiyo ambayo ilitoka kwenye mtandao wa udaku uitwao Gawker.

No comments:

Post a Comment