Ozil Ashinda Tena

Mchezaji mwenye umri wa miaka 25, Mesut Ozil kwa mara ya tatu mfululizo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Ujerumani. Kura zilisimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ujerumani zilimpa kiungo huyo wa Arsenal zaidi ya 30% ya kura zote. Aliongoza juu ya wachezaji wa Bayern, Thomas Muller na Phillip Lahm.

Nyota huyo wa Real Madrid amewashukuru mashabiki wake. Tuzo hii imenipa faraja na furaha. Na juu ya yote sababu (kura) zilipigwa na mashabiki." Alisema.

No comments:

Post a Comment