Mchezaji wa Zamani wa Aston Villa, West Ham na Everton Nyota Thomas Hitzlsperger Ajitangaza Kuwa Yeye ni Shoga

Mchezaji aliyewahi kuzichezea timu za Aston Villa, West Ham na Everton kiungo Thomas Hitzlsperger amefunguka na kuweka wazi kwamba yeye ni shoga.

Ni mchezaji wa kiwango cha juu wa mpira wa miguu kujitokeza na kutangaza wazi kwamba yeye ni shoga mara baada huku akifata nyayo mchezaji toka Marekani Robbie Rogers, ambaye naye alifunguka juu ya hilo hapo mwaka jana.

Hitzlsperger ameshinda mataji 52 akiwa na Ujermani na alimaliza mpira wake akichezea Stuttgart mnamo mwaka jana, akistaafu kutokana na majeraha.

Kwenye mahojiano na Jarida la Time la nchini Ujerumani, alisema: "Kimekuwa ni kipindi kirefu na kigumu... ni hivi tu kwenye miaka ya karibuni nilipoamua kuishi na mwanaume mwengine."

Hitzlsperger, 31, amesema hamfahamu mchezaji mwengine yeyote anayecheza Ujerumani ambaye ni shoga.

Chanzo: SKY Sports

No comments:

Post a Comment