Ex Miss Venezuela na Aliyekuwa Mume Wake Wauwawa kwa Kupigwa Risasi Barabarani

Aliyekuwa Miss Venezuela 2004 ambaye pia ni muigizaji, Monica Spear, 29, na aliyekuwa mume wake Thomas Berry, 39, wameuwawa kwa kupigwa risasi wakiwa barabarani kwenye gari nchini kwao Venezuela na wanaosadikiwa kuwa ni majambazi mbele ya mtoto wao mwenye miaka 5 mnamo siku ya Jumatatu January 6, taarifa za vyombo vya habari vya ndani vimeeleza.

Monica na Thomas walikuwa wanasafiri na mtoto wao usiku wa Jumatatu na gafla gari lao liligonga kitu chenye ncha kaliambacho kilikuwa kwenye barabara ya Puerto Cabello.

Wawili hao waliamua kushuka kwenye gari na kutaka msaada, wakiwa wanasubiri msaada ghafla wakaona watu wenye siraha wakiwa wanakuja kwenye usawa wao, hivyo wakaamua kuingia kwenye gari na kujifungia. Kumbe jamaa walikuwa ni majambazi, wakaanza kufyatua risasi kwenye madirisha ya gari, ambazo zilizowauwa Monica na Thomas huku zikimjeruhi mtoto wao wa kike.

No comments:

Post a Comment