Cristiano Ronaldo Ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora Wa Dunia

Mchezaji wa timu ya Real Madrid na Cristiano Ronaldo ametawazwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka 2013 wa FIFA hii ikiwa ni mara ya pili kushinda tuzo hiyo huku akiwapiku Lionel Messi wa Barcelona na Frank Ribery wa klabu ya Bayern Munich.
Mchezaji huyo nyota wa klabu ya Real Madrid alipata upinzani mkali kutoka kwa Lionel Messi na Frank Ribery kuweza kushinda tuzo hiyo kubwa kabisa duniani.
Cristiano Ronaldo aliwahi kutwaa tuzo hiyo ya mchezaji bora wa Dunia mnamo mwaka 2008 alipokuwa anaichezea klabu ya Manchester United ya Uingereza.


No comments:

Post a Comment