Aliyemwagia Acid Msichana Huyu Hatimaye Akamatwa, Kumbe Alikuwa ni Rafiki Yake

Msichana mwenye umri wa miaka 21, Naomi Oni, alivurugiwa furaha ya maisha mara baada mtu mmoja asiyejulikana akiwa amevaa hijabu kumwagia acid usoni, tukio hilo lilitokea katika kipindi ambacho msichana huyo alikuwa njiani kurudi nyumbani kwake toka kazini mnamo siku ya Jumapili ya December 30, 2012 kwenye Barabara ya Lodge Avenue Dagenham, Mashariki ya jiji la London.
Naomi alimuelezea mtu huyo aliyemshambuli kuwa alikuwa ni msichana aliyevaa vazi la Kiislamu. Kwa zaidi ya mwaka baadae, polisi walifanikiwa kumpata msichana huyo, na alikuwa si mwengine bali ni rafiki yake Mary Konye, 21, ambaye alifanya kitendo hicho kutokana na wivu.

No comments:

Post a Comment