Nyota wa Filamu ya Fast and Furious Paul Walker Afariki kwa Ajali ya Gari

Paul Walker
Nyota wa filamu Paul Walker, ambaye anajulikana sana kuwa mmoja wa washiriki wa filamu ya Fast and Furious, amefariki kwenye ajali ya gari jana Jumamosi.

Ajali hiyo ilitokea Santa Clarita kaskazini mwa Los Angeles alipokuwa njiani kwenda kwenye tukio la kijamii.


Walker alikuwa ni abiria kwenye gari aina ya Porsche ambalo lilipoteza uelekeo na kwenda kugonga kama sio nguzo ya taa au mti na kisha kukatika vipande vipande.


Dereva wa gari hilo pia alifariki.

Habari juu ya ajali hiyo mara ya kwanza ilitangazwa na Mtandao wa Marekani uitwao TMZ, na kifo cha nyota huyo kilikuja kutangazwa na kupitia ukurasa wake wa Facebook, taarifa ilisomeka: “Kwa masikitiko makubwa tunalazimika kutangaza rasmi kwamba Paul Walker amefariki leo kutokana na ajali mbaya ya gari alipokuwa anaelekea kwenye tukio la kijamii kwa ajili ya shirika lake la Reach Out Worldwide.

“Alikuwa ni abiria kwenye gari la rafiki, ambapo wote wawili walipoteza maisha yao, tunaomba uvumilivu wenu, hata sisi tumeshtushwa na kuhuzunishwa na kifo hiki ambacho kinatufanya kama tusiamini habari hii.

“Tunaomba muendelea kuwa na familia na rafiki zake kwa maombi yenu kupitia kipindi hiki kigumu, tutafanya jitihada zote kuwaeleza juu wapi kwa kutuma rambirambi.”


Eneo la tukio

Zimamoto wakiwa kazini

Askari wakiwa eneo la tukio



Mfano wa Gari aina ya Porsche GT alilokuwa  Paul Walker kwa mujibu wa  TMZ.

No comments:

Post a Comment