Moja kati ya kifo kilichotingisha bara la Africa ni cha mwanamuziki nyota toka nchini Nigeria aitwaye Goldie, kifo chake kilitokea mnamo February 14, nchini Nigeria kimeelezwa kuwa ndiyo kifo kilichoshtua watu wengi sana kwa mwaka 2013.
Hakika haikuwa Nigeria peke yake hata na kwa baadhi ya nchi za Afrika Tanzania ikiwa ni mojawapo, Goldie aliwahi kushirikiana na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Ambwene Yesaya maarufu kama AY kwenye wimbo wake uitwao Skibobo.
Pia alikuwa ni mmoja kati ya washiriki wa shindano maarufu la The Big Brother Africa, ambalo lililomfanya afahamike na jamii kubwa ya watu wa Bara la Afrika na Duniani kwa ujumla.
Alifariki kwenye Hospitali ya Reddington iliyopo Kisiwa cha Victoria, Lagos. Kifo kilimkuta katika kipindi alichokuwa amerudi Nigeria toka California, ambapo alikwenda kushuhudia Tuzo za Grammy akiwa na Kenny Ogungbe, ambaye alikuwa ni bosi wa lebo yake iitwayo Kennis Music.
Ilitaarifiwa kwamba msichana huyo alikuwa anajisikia maumivu makali ya kichwa kabla ya kukimbizwa hospitali, na alifariki mara tu baada ya kufika hospitali.
No comments:
Post a Comment