Ahukumiwa Miaka 10 Jela kwa Kumla Uroda Mbuzi, Mbuzi Afika Mahakamani kwa Ushahidi [PICHA & VIDEO]


Jamaa mmoja mwenye umri wa miaka 28 amehukumiwa kwenda jela miaka kumi mara baada ya kukutwa na hatia ya kufanya tendo la ngono na mbuzi.

Katana Kitsao Gona toka Malindi nchini Kenya wiki iliyopita alikiri kufanya ngono na mnyama. 


Shuka chini kuangalia Video hiyo..... Mbuzi huyo wa kike kwa utulivu alikuwa pembeni ya chumba cha mahakama wakati hukumu hiyo ilipokuwa inatolewa. Jamaa huyo alikamwatwa mnamo tarehe 25 Novemba mara baada ya mkazi mmoja wa eneo hilo kumbamba akiwa uchi wa mnyama akimla uroda mbuzi huyo ambaye alikuwa amefungwa kamba, hii ni kwa mujibu wa The Star.



Mmiliki wa mbuzi huyo alifahamishwa na kufika eneo la tukio akiwa na majirani wengine ambao pia walimshuhudia Gona akiwa anafanya ngono na mnyama.

Jamaa alikamatwa na polisi na vipimo vya hospitali vinakaonyesha kweli kwamba tukio la ngono lilifanyika.



Gona aliomba msamaha kwa mahakama kwa kujitetea kuwa mke wake ni mlemavu na anamtegemea yeye ila mahakama ikajibu kuwa kosa hilo ni kubwa na akapewa siku 14 za kukata rufaa.

Angalia Video hapo chini..




Una habari au stori na ungependa itoke kwenye blog hii? Tafadhali nitumie kwa E-mail: danchibo@yahoo.com

No comments:

Post a Comment