Zlatan Ibrahimovic: Sitofuatilia Mashindano ya Kombe la Dunia

Zlatan Ibrahimovic
Kapteni wa timu ya taifa ya Sweden Zlatan Ibrahimovic anasema hatoyafuatilia mashindano ya kombe la Duna mara baada ya kutopata nafasi ya kushiriki kwenye michuano hiyo baada ya kufungwa kwenye mechi yao dhidi ya Ureno hapo jana.

Mshambuliaji huyo wa Paris St-Germain alifunga magoli mawili kwenye mechi iliyofanyika siku ya Jumanne ila magoli matatu yaliyofungwa na Cristiano Ronaldo iliwezesha Ureno kupata nafasi ya kushiriki michuano hiyo kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-2. 

Ibrahimovic, 32, alisema: "Kitu kimoja kwa hakika, kwangu mimi binafsi sitoifuatilia michuano ya Kombe la Dunia. 

"Hongera zangu kwa ureno, ila timu hizi mbili zilistahili kwenda kwenye Kombe la Dunia." 

CHANZO: BBC Sports

No comments:

Post a Comment