Uruguay Yawa Nchi ya Mwisho Kupata Tiketi ya Ushiriki wa Kombe la Dunia


Uruguay imekuwa nchi ya mwisho kupata tiketi ya ushiriki wa mashindano ya kombe la Dunia yatakayofanyika nchini Brazil hapo mwakani mara baada ya kutoka sare ya 0-0 kwenye mechi yao ya marudio dhidi ya Jordan.

Licha ya kutoshinda mechi hiyo Uruguay walifanikiwa kutawala mchezo huo huku wakijivunia akiba ya magoli 5-0 waliyoyapata kwenye mechi yao ya kwanza.

"Tunafuraha sababu ukweli ni kwamba ilikuwa ni njia ngumu," alisema mshambuliaji wa timu hiyo Edinson Cavani.

No comments:

Post a Comment