Misri Yampiga Chini Kocha Wake Bob Bradley

Bob Bradley
Mwenyekiti wa Shirikisho la soka nchini Misri Gamal Allam ametangaza kuwa Bob Bradley sio kocha tena wa timu ya taifa ya nchi hiyo mara baada ya timu hiyo kushindwa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.

Mkataba wa Bradley umekwisha mara baada ya kushindwa kwenye kampeni za ushiriki wa kombe la Dunia mnamo siku ya Jumanne dhidi ya Ghana kwa jumla ya mwastani wa magoli 7-3 hivyo hatokuwa kocha wa mafarao hao.


“Mkataba wa Bob Bradley umeisha usiku usiku huu, na hatutaingia tena kwenye mkataba mwengine, tutaanza kutafuta kocha mwengine. Nadhana Bradley hatokubali kuendelea kubaki hapa mara baada ya kupoke shutuma nyingi kutoka kwenye vyombo vya habari mara baada ya mechi ya iliyofanyika  Kumasi.


No comments:

Post a Comment