UNYAMA: Mwanamke Auwawa Kikatili na Kutupwa Kwenye Ndoo ya Taka (PICHA)


Polisi wa kitongoji cha Mile 7 wameikuta maiti ya msichana mmoja aliyeuwawa kinyama kisha mwili wake kutupwa kwenye kwenye ndoo ya kuhifadhia taka karibu na Shule ya Morning Star pande za Tantra Hill, nchini Ghana.

Mwili wa Marehemu huyo ambaye hakufahamika na watu, ulikutwa kwenye ndoo ya kuhifadhia uchafu kwenye makazi ya watu ukiwa umefunikwa na kutupwa kwenye ndoo hiyo ya taka huku ndoo hiyo ikiwa imefungwa na kugongelewa misumari ya nchi nne kwa pande zote. 

Kulikuwa na alama za kupigwa na kuteswa kwenye mwili ambazo inaaminika zilizotokana pia na kitendo cha kuulazimisha mwili huo kuingia kwenye ndoo hiyo ya taka.

DSP Peter Yembillah, ambaye ni Kamanda wa kitongoji cha Mile 7, ambaye aliongoza msafara kwenda kwenye eneo la tukio mapema jana alfajiri, alilieleza gazeti la DAILY GUIDE la nchini humo kwamba ni dhahili mwili huo ulitupwa kwenye eneo hilo na waliohusika na kifo cha mwanamke huyo.

No comments:

Post a Comment