Beyonce ni Mjamzito Akitegemea Kupata Mtoto wa Pili

Imetaarifiwa kwamba Beyoncé na Jay-Z wanategemea kupata mtoto wa pili. Vyanzo mbalimbali vimeeleza ikiwemo E! Online huku ikisema kwamba mwimbaji huyo kwa sasa ni mjamzito.

Taarifa juu ya uwezekano wa Beyonce kuwa na ujauzito zilianza kuenea hivi karibuni mara baada ya mwanamuziki huyo kuahirisha tamasha lake alilotakiwa kulifanya nchini Belgium kwa kile kilichoelezwa kimetokana na ushauri wa daktari huku akitakiwa kupata mapumziko ya kutosha.


Beyonce amekuwa akisikika mara kwa mara akisema kuwa anahitaji kupata mdogo wa Blue Ivy. “Ningependa kupata watoto zaidi. Nafikiri mtoto wangu anahitaji kampani. Binafsi napenda kuwa dada mkubwa… kwa namna flani, inapotakiwa kutokea,” aliieleza  ABC News.


Nitaendelea kukutaarifu zaidi juu ya habari hii itakavyokwenda

No comments:

Post a Comment