Pope Francis Amuonya Mchezaji wa Italia Mario Balotteli

Pope na Balotelli
Hivi karibuni Pope Francis aliwapa somo nyota wa mpira wa miguu akiwemo Lionel Messi na Mario Balotelli juu ya majukumu yao, akiwaeleza “hakuna nafasi ya mtu mmoja mmoja”.

Pope aliongea na wachezaji hao wa timu za Taifa za Italy na Argentina jijini Vatican kwenye mkesha wa mechi ya kirafiki baina ya timu hizo mbili jijini Rome.

Aliwaambia alikuwa yupo njia panda juu ya timu ya kuishangilia, akisema: “Itakuwa ni ngumu kwangu, ni bahati nzuri tu ni mechi ya kirafiki! Na tuwe na hakika kwamba ipo hivyo.”

Pope mwenye umri wa miaka 76, ni mshabiki wa muda mrefu wa klabu toka Argentina iitwayo San Lorenzo, aliwataka wachezaji wa timu hizo kuhakikisha wanatumia umaarufu wao kuonyesha mifano bora kwa mashabiki wao.

“Ninyi, wachezaji wapendwa, ni mashuhuri sana. Watu wanafata mifano yenu, ndani na nje ya uwanja. Mna majukumu ya kijamiii”.
 
Pia alimtania mchezaji wa AC Milan, Balotelli, ambaye mara nyingi amekuwa akiandikwa kwenye vichwa vya habari kutokana na tabia mbaya, akisema: “Hapa Vatican, wananiambia kwamba mimi sina nidhamu!”
Pope Akiwa na Messi na Buffon

Pope Akiwa na Wachezaji wa za Taifa za Italia na Argentina

No comments:

Post a Comment