Maswali ya Msingi Kujiuliza Juu ya Huyu Trafiki Feki


Hii habari ya yule trafiki feki aliyekamatwa na kudai alifanya kazi hiyo kwa miaka kumi na tano na kwamba alirithi sare kutoka kwa ndugu yake, inanipa maswali ambayo ningependa unisaidie majibu yake:-

1. Kwa miaka yote hiyo ni kwamba zile sare zilikuwa hazichakai ama..?
2. Kwa miaka yote hiyo imewezekana vipi afanye kazi hiyo pasipo kujulikana na alitumia mbinu gani kufanikisha utapeli wake...?
3. Kwa miaka yote hiyo alikuwa anasimama barabarani peke yake na jeshi la polisi lilikuwa wapi kushindwa kumbaini mfanyakazi wao feki...?
4. Je unadhani anastahili adhabu au labda anahitajika kuongezewa elimu ya utrafiki ili aendeleze fani maana kaonyesha kuwa ana vipaji vingi..?
5. Na je kama huyu kabainika je unadhani ni wangapi wa aina yake watakuwa wameenea mabarabarani ambao mpaka sasa hawajabainika...?
6. Jeshi la Polisi tunaliweka kwenye nafasi gani kutokana na ishu hii...?

No comments:

Post a Comment