Kanye West Anunua Gari Mbili za $1.2 Million Kila Moja Ili Kuilinda Familia Yake (PICHA)


Kwa mujibu wa taarifa, Kanye West ametumia kiasi cha $1.2 million kila moja kwa ajili ya ya kununulia magari mawili za kuwalinda Kim K na mtoto wao wa kike, North.

Gari hilo la chuma lenye rangi ya dhahabu ambalo linalotengenezwa na Dartz Motorz (kwenye picha juu) linasemekana kuwa lina mazingira yanayosaidia kukwepa vitendo vya utekwaji, uporwaji na aina nyinginezo za matatizo ambayo mara nyingi huwapata watu matajiri mitaani'

Gari hii imetengenezwa kwa namna ambayo hata likipigwa na mabomu madogo kama aina ya grenade lina uwezo wa kustahimili mikiki yake.

'Kanye anafahamu fika familia yake mpya inaangaliwa na wengi, na malengo yake ni kuhakikisha anayapata magari hayo mapema na hasa lile la Kim katika kipindi ambacho atakuwa hajaanza ziara yake ya kimuziki ndani ya US ndani ya mwezi October,'  chanzo kiliieleza Daily Star.

No comments:

Post a Comment