Brandy Aimba Kwenye Uwanja Mtupu

Brandy
Mwanamuziki Brandy alipangwa kufanya show ya kushtukiza pasipo watu kupewa taarifa yoyote kwenye Siku ya Nelson Mandela ya Michezo na Utamaduni, ila kutokana na mashabiki kutokuwa na taarifa karibia wote walitoka uwanjani hapo kwenye muda ambao mwanamuziki huyo alipopanda jukwaani.

Kwa kukumbusha tu ni kwamba, uwanja wa FNB uliopo Soweto, Afrika Kusini ulikuwa na wageni 90,000 waliofurika kwa siku nzima. Brandy alipojitokeza kwenye wakati wake muafaka ni watu kama 40 pekee waliokuwa wamebaki.

"Brandy ameimba kwenye uwanja mtupu. Huku taa zikiwa zimewaka uwanjani hapo," mwanamuziki Kabomo ali-tweet.

Uwanja wa FNB
Kutokana na hali hiyo inaelezwa kwamba Brandy hakuweza kuimba kwa muda mrefu. "Watu hawakuwa wanafahamu kwamba kutakuwa na tamasha baada ya michezo. Hakuna aliyekuwa anajua kwamba Brandy alikuwepo. Labda watu 40 ndio walishuhudia," Kabomo aliandika kwenye mtandao wa kijamii. "Alisitisha kuimba na kuondoka baada ya kuimba nyimbo mbili tu".

No comments:

Post a Comment