Papa Francis Asema “Mimi ni Nani Kuwahukumu Mashoga?"

Papa Francis
Papa Francis amesema watu ambao ni mashoga hawatakiwi kutengwa na jamii.

Akiongea na waandishi akiwa anamaliza ziara yake nchini Brazil, Papa alisema msimamo wa Kanisa Katoliki ni kwamba sheria ya ushoga ni sio kitu kizuri na ni dhambi.

“Kama mtu ni shoga na anamuomba Mungu na anamaanisha, mimi ni nani kumuhukumu ?” Alisema Papa Francis.

Pia alisema alihitaji kuona nafasi kubwa kwa wanawake Kanisani, ila hawawezikani kwa wao kuwa  Wachungaji.

No comments:

Post a Comment