Kelly Rowland Aokolewa Baharini Baada ya Kupotea kwa Masaa 12

Kelly Rowland
Mwanamuziki wa miondoko ya R&B, Kelly Rowland ameokolewa kwenye bahari mara baada ya kukwama baharini kwa masaa 12.

Rowland akiwa na watu wengine kadhaa walikutwa na kisanga hicho wakati wanashuhudia maonyesho yaliyofanyika ndani ya boti moja mnamo siku ya Ijumaa asubuhi (July 19th) na gafla hali ya hewa ikabadilika na kusababisha mawimbi makali.

Kepteni wa boti hiyo alipatwa na wasi kutokana na hali ilivyobadilika, ila kepteni wa wa boti ya TowBoat U.S. aitwaye Noah Santos alifanikiwa kumuokoa kila mmoja aliyekuwa kwenye boti hiyo akiwemo mwanamuziki huyo wa ngoma ya “Sail On”.

Santos alisema “kila mmoja alikuwa anatetemeka.” Na baada alipokea asante ya moja kwa moja toka kwa Kelly Rowland:

“Tulitoka naye siku inayofuata nikiwa na mke wangu kisha akatununulia chakula cha usiku. Aliniambia kwamba mimi ni shujaa wake.”


Mpaka sasa aakuna kauli yoyote toka kwa Kelly Rowland au timu yake kutokana na tukio hilo.

Hebu cheki picha ya Kelly akiwa na muokozi wake, Noah Santos..

No comments:

Post a Comment