Watoto Watatu Wazaliwa Ndani Ya Miezi Tisa, Wana Umri Sawa Ila Sio Mapacha Watatu

Carra, Laura na Jenna I
Wote ni watoto wa tumbo moja, na wote wana miaka minne ila hawajazaliwa kama mapacha watatu.

Wa kwanza anaitwa Cara, akiwa na miezi minane tu ndipo alipokuja kuwa mkubwa kwa kubahatika kupata wadogo zake wawili ambao ni mapacha, Laura na Jenna.

Mama yake, Tessa Singh, 40, alipata mimba wiki 12 baada ya yeye kuzaliwa, na mapacha wakaja kuzaliwa wakiwa njiti wiki 28 baadae.

Hii ina maana kwamba, katika miezi mitatu ya kila mwaka watoto hawa hulingana umri.
Mrs Singh alisema: ‘watu huwa hawaamini pale ninapowaambia kwamba watoto hawa wana umri mmoja licha ya kwamba sio mapacha watatu.
Carra, Laura na Jenna I

Wakiwa Na Wazazi Wao

No comments:

Post a Comment