Mwili wa Mangwea Kuletwa Nchini Jumamosi na Kuzikwa Jumatatu Morogoro

Adam Juma
Wakati  Watanzania wakiendelea kuomboleza msiba wa msanii wa miondoko ya Hip Hop Albert Mangwea Msemaji wa Kamati ya Inayoshughulikia msiba huo Adam Juma amesema mwili wa Marehemu unategemea kuja nchini siku ya Jumamosi.

Kwenye maongezi niliyofanya nae leo hii Adam alisema kama mipango itakwenda sawa  basi wanategemea mwili wa Marehemu kufika nchini siku ya Jumamosi, “kama vitu vitaenda sawa mwili wa marehemu utafika Jumamosi na ukishafika utaenda kuhifadhiwa" alisema Adam.


Akaendelea kwa kusema “Jumapili ndio tutafanya Last Respect, kwa maandalizi ya awali hiyo last respect tunaweza kuifanya pale Kijitonyama Viwanja vya Posta, hiyo itakuwa ni kuanzia saa mbili mpaka saa 10, baada ya hapo mwili utasafirishwa kuelekea Morogoro na kuzika siku ya Jumatatu” alimaliza Adam.

No comments:

Post a Comment