Bobby V Aomba Radhi kwa Mziki Wake: Asema Nimekuwa Siwatendei Haki

Bobby V
Nimekuwa "nikizisaka radio zaidi ya ambavyo nimekuwa nikisaka mawazo na mioyo ya watu" amekiri muimbaji Bobby V. Kwa sasa amerudi akiwa kwenye harakati za kupromoti single yake mpya iitwayo “Back to Love”.

Ana album tano mpaka sasa, na muimbaji huyu wa ngoma ya “Slow Down” Bobby V anajaribu kufanya kitu tofauti.


Kwenye video yake mpya mwanamziki huyo anasema “Najihisi kama siwatendei watu haki”,  akijaribu kulinganisha na mziki wake wa siku za nyuma.

Anaamini ni muda wa kurudi kwenye mizizi, na utaona kwenye video, Mr. V huku akiwa anapiga kinanda.

No comments:

Post a Comment