Beckham Awanunulia Magari Mama Na Mkwe Wake Kama Zawadi Ya Kuwashukuru Kutunza Watoto Wake

Sandra na Jackie wakiwa na Watoto wa Beckham
DAVID Beckham amenunua magari mawili yenye thamani ya Paundi 30,000 kwa mama yake mzazi na mama mkwe wake katika hali ya kuwashukuru kwa walivyomsaidia katika kipindi chote alichokuwa anacheza mpira.
 
Wiki iliyopita Becks, 38, alinunua gari za aina ya Audi Q3s na kuzituma moja kwa mama yake aitwaye Sandra na lingine kwa mama wa mke wake Victoria aitwaye Jackie Adams.

Zilikuwa ni zawadi za kushtukiza katika kuwashukuru kwa kwa jinsi walivyoweza kuwasaidia kwa miaka yote kuwalea watoto wao na kuzunguka nao pande mbalimbali za Dunia, hii yote ni katika hali ya kumuunga mkono yeye na mkewe Posh, 39, katika kipindi ambacho kazi zao ziliwataka waende mbali.

Magari ya Sandra na Jackie

No comments:

Post a Comment