Rooney Aongoza Kwa Utajiri Miongoni Mwa Wachezaji Wa EPL

Wayne Rooney
Mchezaji wa timu ya Manchester United na mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Uingereza Wayne Rooney, anatajwa kuwa ndiye mchezaji tajiri kuliko wote kati ya wanaocheza kwenye Ligi Kuu ya Uingereza kwa sasa.
 
Kwa mujibu wa gazeti la The Sunday Times kwenye orodha yake ya wachezaji matajiri wanaocheza kwenye Ligi hiyo kwa sasa, utajiri wa Rooney unakadiliwa kuwa ni paundi za Uingereza millioni 79.01.

Jumla ya wachezaji ishirini na nne wanaocheza kwenye ligi kuu ya Uingereza ni miongoni mwa wanamichezo 100 tajiri wa Britain na Ireland.
 
Utajiri wa Rooneys umepanda kwa paundi millioni sita kutoka mwaka 2012 huku akichanganya na utajiri wa mke wake Coleen ambae utajiri wake unakadiliwa kufika paundi millioni 64.

Mchezaji mwenzake wa United, Rio Ferdinand anashika nafasi ya pili, akiwa na utajiri wa paundi millioni 42 huku mshambuliaji wa klabu ta Stoke City Michael Owen akiwa ni wa tatu kwa kuwa na utajiri wa paundi millioni 38.

Utajiri huo umepimwa kwa mali zinazotambulika kama ardhi, thamani pamoja na hisa mbalimbali zilizopo kwenye makampuni.

Nahodha wa zamani wa Uingereza David Beckham, ambaye kwa sasa anaichezea Paris St Germain, anashika nafasi ya 11 ya matajiri michezo wa dunia iliyotajwa na gazeti hilo la Sunday Times, huku akikadiliwa kuwa na utajiri wa paundi millioni 165.

Mchezaji namba moja wa mchezo wa gofu Duniani Tiger Woods ndiye anayeshika nafasi ya kwanza huku utajiri wake ukikadiliwa kuwa wa paundi millioni 570.

Hii orodha ya Wachezaji 10 Matajiri wanaocheza kwenye Ligi Kuu ya Uingereza kwa sasa:

1. Wayne Rooney (Manchester United) paundi millioni 51

2. Rio Ferdinand (Manchester United) paundi millioni 42

3. Michael Owen (Stoke City) paundi millioni 38

4. Ryan Giggs (Manchester United) paundi millioni 34

4. Frank Lampard (Chelsea) paundi millioni 34

6. Steven Gerrard (Liverpool) paundi millioni 33

7. Fernando Torres (Chelsea) paundi millioni 26
8. John Terry (Chelsea) paundi millioni 24

9. Joe Cole (West Ham United) paundi millioni 21

10. Petr Cech (Chelsea) paundi millioni 20
 


(Paundi 1 =  Shilingi 2500)

No comments:

Post a Comment